Wakili wakujitegemea Hamis Ramadhani
Kimilomilo amewaasa wananchi kuepuka tamaa za Mali pale mmiliki anapofikwa na umauti.
Ameyasema hayo Ofisi kwake wakati
akifanya mahojiano na Buha FM radio leo juu ya umuhimu wa kuandika mirathi na
kusema kuwa wapo baadhi ya wananchi wanaokiuka mirathi iliyoachwa na mmliki
baada kufariki jambo ambalo linakuwa chanzo cha migogoro ndani ya familia
"Unapo kiuka na kuingiza tamaa
ya Mali inakuwa chanzo cha ugomvi na wengine kujichukulia sheria mkononi kuua
au kujeruhi Moja kwa moja unakumbana na adhabu ya makosa ya mauaji au kujeruhi
"alisema Wakili Kimilomilo.
Wakili Kimilomilo amesema upo
umuhimu wa kuandaa mirathi kwa wamiliki wa mali kwakuwa inasaidia kuepuka
migogoro ya kifamilia.
"Wananchi ondoeni hizo kasumba
kwamba ukiandaa mirathi unajichulia kifo hapana tambua kuwa mali hizo umetafuta
kwaajili ya familia unapofariki bila mchanganuo wowote inatengeneza migongano
ya kifamilia hasa ukikutana na watoto au ndugu wenye tamaa"Ameongeza
Wakili Kimilomilo.
Godhope Isaya,Erick Erick na Samwel
Kajula ambao ni wananchi Kasulu Mji Mkoani Kigoma wamesema kuwa umuhimu upo wa
kuandaa mirathi kwasababu inasaidia kupunguza kesi mahakama za mwanzo, Baraza
la ardhi na kuepusha mfarakano ndani ya familia.
"tunashudia kesi nyingi za mirathi
katika mabaraza ya ardhi na hata mahakama za mwanzo na chanzo chake nikutokuwa
na uwazi wa mali anazo miliki baba au Mama kwenye familia inapotokea kifo
migongano na chuki zinaibuka kwenye familia" walisema Wananchi.
Wananchi hao wameiomba Serikali na
mahakama kutoa elimu kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuwajengea wananchi uwelewa
wa mirathi.
" Tunaomba Serikali kupitia
bunge wasisitize kuhusu sheria ya mirathi lakini mahakama zetu pia watoe elimu
kupitia vyombo vya habari kwani tunaamini kuwa wapo wenzetu ambao hawajui, hawajawahi
kusikia juu ya umuhimu wa jambo kama hilo" waliongeza wananchi.
Mahakama ya mwanzo kasulu Mji katika
kipindi cha mwaka 2024 zimefunguliwa kesi zaidi ya 60 zinazohusiana na mirathi.
Muandishi : Eunice Jacob.
Mhariri : Mussa Mkilanya.
0 Comments