Ajali za mwisho wa mwaka kukomeshwa Kasulu

Mkuu wa usalama Barabarani wilayani Kasulu Mlakibu Msaidizi wa Polisi Patirck Damas amewaagiza wafanyabiashara ya usafirishaji Abiria malufu Bajaji kufata Sheria  za usalama barabarani ili kupunguza ajari zinazojitokeza mwisho wa mwaka.

Akizo hilo amelitoa leo wakati akizungumza na madereva Bajaji katika eneo la stendi mpya wilayani kasulu huku akiwataka kupata mafunzo ambayo yamekuwa yakitolewa ili wawezekupata vyeti vitakavyowasaidia kupata Leseni za udereva wa vyombo vyao.

“Ili tuweze Kwenda vizuri kwenye hii sikukuu lazima tufuate sheria na kanuni za barabarani kwa sababu muda huu safari zinakuwa zinahitajika kwa kiasi kikubwa sio mizigo sio abiria sasa haitupi nafasi ambayo itatufanya tuvunje sheria na wale waliofunga viti pembeni kwenye bajaji zao mkavitowe kama huna leseni tafuta leseni fanya kazi yako” Amesema Kamanda Damas.


Mkuu wa usalama Barabarani wilaya ya Kasulu Mlakibu Msaidizi wa Polisi Patirck Damas

Aidha kwa upande wake katibu wa waendesha Bajaji Hamis Juma Mkuyu amesema watatekeleza kile kamanda wa usalama barabarani alichowaagiza huku akitaka mafunzo yawe yanatolewa kila wakati ili kuwasaidia Madereva Kubadilika na kupata elimu inayotolewa.

“Naungana na kile alichokisema mkuu wa usalama barabarani aliyoyazungumza ni sawa kabisa na nimshukuru lakini naomba elimu hii iendelee kutolewa kila mara kwani madereva ni watu wa kubadilika lakini nitaendelea kushirikiana na viongozi wenzangu kuhakikisha matukio ya ajari barabarani yanapungua kwa kufuata sheria za usalama barabarani” Amesema Mkuyu.

Baadhi ya dereva bodaboda kasulu wakipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa usalama Barabarani wilayaani Kasulu Mlakibu Msaidizi wa Polisi Patirck Damas

Bilali Bakari ambaye ni mwendesha bajaji na mwenyekiti wa nidhamu katika kijiwe cha Bajaji Mnadani amesema madereva wanatakiwa kufauata taratibu na sheria zilizowekwa na vijiwe ili kupunguza matukio na changamoto zinazojitokeza katika vijiwe hivyo.

“Mimi kama mwenyekiti wa nidhamu kijiwe cha bajaji Mnadani nimewambia ni marufuku bajaji inayotoka mjini haitakiwi kupaki mkono wa kushoto inatakiwa ipaki mkono wa kulia nimeongea nao wote na wamenisikiliza na abiria anapoona bajaji inawatu watatu wanne asipande kwani huo ni uvunjifu wa sheria za barabarani” Amesema Bilali.

Mkuu wa usalama Barabarani wilayaani Kasulu Mlakibu Msaidizi wa Polisi Patirck Damas akitoa mafunzo na maelekezo kwa dereva bajaji kasulu

Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na chuo cha VETA Nyumbigwa limekuwa likitoa mafunzo kwa madereva wa vyombo vya moto hasa Bajaji na Pikipiki ili kupunguza ajari zinazopelekea kupoteza Maisha na ulemavu wa kudumu kwa raia wengi nchini.

Mwandishi; Sharfati Shinji
Mhariri; Ramadhan Zaidy

Post a Comment

0 Comments