Wabunge zaidi ya 15 na maafisa wengine watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamenusurika kifo kutokana ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Shabiby na Lori la Mizigo wakati Wabunge hao wakielekea kwenye Mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge, imesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi, Desemba 6.2024, maeneo ya Mbande, Kongwa, mkoani Dodoma baada ya basi hilo kugongana na lorila mizigo.
Majeruhi wa ajali hiyo ambao ni maafisa wa Bunge waliokuwa ndani ya gari hilo wamepelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamin Mkapa, mkoani Dodoma, huku taarifa za kina kuhusu hali zao zikiwa hazijatolewa rasmi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia dereva wa gari la Kampuni ya Shabiby lenye namba za usajili T 149 EGM aina Yutong aliyejulikana kwa jina la Bahati Said Juma (42) kwa uzembe wa kusababisha ajali hiyo.
.Mwandishi:Harieth Dominick.
0 Comments