Chama Cha Mapinduzi chawashukuru wananchi Kigoma

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma cde.Jamal Tamim amewashukuru wananchi wa mkoa wa kigoma kwa kukichagua chama cha mapinduzi katika uchaguzi uliopita.

Ametoa shukrani hizo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya kibondo community center mjini Kibondo ambapo amesema baada ya ushindi jukumu la viongozi hao ni kutenda haki kwa kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi.

Kwa upande wake katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Cde.Christopher Palangyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa na kwamba chama kitahakikisha wanatimiza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni panoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo, ulinzi na usalama na kusoma mapato na matumizi ya kijiji kila mwaka.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwezi uliopita CCM ilipata ushindi wa zaidi ya asilimia 96 baada ya kushinda vijiji 293 kati 306    , Mitaa  170  kati   176 na Vitongoji    1716   kati ya 1858 .

Post a Comment

0 Comments