Mratibu wa mikopo katika Halmashauri ya mji Kasulu Bwn. Godfrey
Jeremiah ambae pia ni Afisa maendeleo Halmashari ya mji Kasulu amewatoa hofu
wakazi wa Kasulu kuhusiana na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.
Akizungumza na Buha fm katika kipindi cha darasa nje ya
shule leo ameeleza kuwa kuwekuwa na taarifa potofu kuwa usajili wa vikundi
unafanyika kwa udanganyifu na kwamba tayari wapo watu ambao wamesha andaliwa
kupewa mikopo hiyo jambo ambalo sio la kweli.
Ameeleza kuwa mikopo ya Halmashauri bado inatolewa na elimu juu ya mikopo hiyo pia inaendelea kutolewa kwa vikundi mbalimbali kupitia kata husika.
“Ikitokea mtu au kikundi kinahitaji uelewa kuhusu namna ya kuandaa
na kusajili kikundi chao wasisite kututafuta kwa maana kila kata ina afisa
aendeleo ya jamii ambae miongoni mwa majukumu yetu ni kutoa elimu kwa jamii
lakini pia kufatilia maendeleo ya kikundi husika kabla na baada ya kupata
mkopo,” amesema Godfrey.
Kauli ya hiyo ni baada ya kuwepo baadhi wa wakazi wa Halmashauri
ya mji Kasulu hasa wanawake kuelezea kuhusu ukosekanaji wa elimu juu ya mikopo
hiyo na kupelekea kuamini kwamba kufuata taratibu za kusajili vikundi kisheria
ni kupoteza muda.
Mikopo ya Halmashauri ni mikopo ambayo ni asilimia 10% ya mapato
ya Halmashauri husika na inatolewa kwa makundi
maalumu ya wanawake, vijana pamoja na walemavu kwa kuzingatia
muongozo wa kikundi husika.
Mwandishi: Ellukagha Kyusa.
Mhariri : Mussa Mkilanya.
0 Comments