Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Ibrah class amewaasa mabondi wanaochipukia kuwa wavumilivu katika mchezo wa Ngumi, huku akisisitiza kujituma katika mazoezi na kucheza mchezo kwa uwezo wao.
Hayo ameyasema
jana wakati akizindua Kampuni iliyochini yake ya uendeshaji mchezo wa ngumi
aliyoipa jina la King Class Sports.
Bondia huyo
ameongeza kuwa kampuni hiyo imedhamiria kuibua na kuendeleza vipaji vya
mabondia wazawa kwani kampuni yake imejipanga kukabiliana na kuondoa changamoto
zote ambazo wanakutana nazo mabondia wengi wa changa hapa nchini.
“Sasa nimepiga
hodi katika Upromata, mabondio tumekuwa tukizulumiwa sana katika mchezo huu,
wakati mwingine hapewi hata mapambano japokuwa tunajiandaa na kuwa tayari
kucheza hivyo unajikuta unatumia muda mrefu kuonesha kipaji chako, hili
halitakuwepo King Class Sports,” amesema Ibrah.
Aidha Bondia huyo ameongeza
kuwa sikuzote mwanzo ni huwa ni mgumu lakini King Class Sports imejipanga kusaidia
vipaji vya ngumi kucheza ndani ya Tanzania na Nje ya Tanzania.
Bondia Ibrah ametambulisha
mabondia watatu ambao wameingia mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi na
kampuni hiyo ambao ni Issa Mollel bondia Mmasai, Rahimu Khalid Omary na Jawabu
Habibu Kinyogoli.
Bondia Ibrah Class
kwa sasa Tanzania ni Bondia wa pili kwa ubora amecheza mapambano 38 kati ya mapambano
hayo ameshinda mapambano 28 na mapambano 15 ameshinda kwa KO.
Mwandishi: Mussa Mkilanya.
0 Comments