Jeshi la Polisi Wilaya ya Kasulu limetoa wito kwa madereva Bajaji na Pikipiki maarufu kama Bodaboda kuhudhuria mafunzo mara kwa mara kwani ni muhimu kwa kuwa wao ni watumiaji wakuu wa barabara.
Akizungumza leo na Buha FM Radio Mrakibu Msaidizi wa
Polisi Partirck Damas Wilaya ya Kasulu amesema Chuo cha Veta kimeandaa mafunzo
kwa madereva wa Bajaji na Pikipiki lakini ushiriki wa walengwa ni mdogo sana.
Amesema pamoja na uchache wa walengwa bado mafunzo
yametolewa kwa waendeshaa Bajaji na Pikipiki ili kusaidia
kupunguza idadi za ajali barabarani katika wilaya ya Kasulu .
“Mwitikio sio mkubwa kutokana na msimu huu wa kilimo
lakini kwa upande wa Polis tutaendelea kutimiza malengo yetu, na lengo la
msingi ni kutoa elimu kwa vijana waliojisajili waliopo vijiweni ili waelewe
umhimu wa mafunzo na kupata leseni pia tunafanya oparesheni mbalimbali kwa wale
wanaokaidi tutawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria”Ameseama Mrakibu Damas.
Aidha kwa upande wake Mwalimu Mustapha Mussa Mhando
kutoka chuo cha ufundi VETA Nyumbigwa amesema mafunzo waliyoyatowa yameenda
vizuri licha ya kuwa na idadi chache ya madereva huku akitoa wito kwa Madereva
kujitokeza zinapotoka furusa za kujifunza ili kujua matumizi fasaha ya barabara
na kuepuka ajali za barabarani.
“Nafasi bado zipo tunawahitaji nia yetu nikuwasaidia
ili kupunguza ajali nakuwaelimisha juu ya vyombo wanavyovitumia si kwa
wanaotumia tu kwa biashara hata wale wenye vyombo binafsi tunawakaribisha sana
waje wajifunze namna ya kutumia na kuvitunza vyombo vyao vya moto” Amesema Mwl.
Mhando.
Baadhi ya Madereva Bajaji na Pikipiki maarufu Bodaboda Wilaya ya Kasulu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo.
Kwa upande wake mwenyeketi wa waendesha Bajaji Kasulu
mjini Ndg. Liberatusi Kubila amekiri kuwepo kwa mwitikio mdogo kwa madereva
huku akitaja madereva wengi hawajali juu ya mafunzo yanayotolwa licha ya kutoa
taarifa huku akichukizwa na mwitikio mdogo.
“Mwitikio umekuwa mdogo kulingana na uchumi pamoja na madereva kutojali, Nimetoa fomu 60 kwa ajili ya washiriki lakini ukitazama mwitikio ni mdogo na sijafurahishwa, nitowe rai kwa wale ambao hawajafika pale tutakapotangaza wajitokeze kwa wingi ili wapate mafunzo haya” Amesema Ndg. Kubila.
Katika hatua nyingine wakizungumza madereva wa vyombo vya moto akiwemo Piludas Grayani ambaye ni mwendesha Bajaji na Abdul Ramadhani Issa mwendesha pikipiki ya abiri wameeleza namna
walivyonufaika na mafunzo hayo huku wakitaja njia
walizopewa namna ya kulinda vyombo vyao vya moto pamoja na kujilinda wao anapokuwa barabarani.
“Kuna mambo mengi tuliyojifunza hasa mnamna ya kutunza
vyombo vyetu vya moto kwani chombo kikiwa kibovu kinaweza kusababisha ajali pia
alama za barabarani tunaziona ila tulikuwa hatuelewi namna ya kuzitumia hivyo
kupitia mafunzo haya tunaenda kuwa mfano wa madereva bora barabarani” Wamesema
baadhi ya Madereva hao.
Ifahamike kuwa Mafunzo hayo yamedumu kwa siku tano
toka Novemba 2 na kuhitimishwa jana Novemba 6 mwaka huu yakiwa yamejumuisha
wafanya biashara ya usafirishaji abiria bajaji na Pikipiki katika wilaya ya
Kasulu chini ya Chuo cha Veta Nyumbigwa kwa kushirikiana na Jeshi la Usalamaa
Barabarani Wilayani Kasulu.
Mwandishi;
Sharifat Shinji.
Mhariri;
Mussa Mkilanya.
0 Comments