Mwasisi na mtendaji mkuu wa kituo cha habari cha Buha FM Radio inayopatikana Mwilamvya, Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Ndg. Prosper Kwigize amechaguliwa kushika nafasi ya ujembe wa Bodi ya uongozi wa Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN).
Katika uchaguzi huo uliofanyika
Novemba 04 mwaka huu jijini Dodoma Ndg. Kwigize amepata kura 31, akifuatiwa na
Alex Benson Sichona kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam aliyepata kuwa 28.
Aidha kwa upande wa Mwenyekiti
wa Misa-Tanzania Ndg. Edwini Soko ameshinda nafasi hiyo akipokea kijiti kutoka
kwa Salome Kitomari ambaye alikuwa mwenyekiti wa taasisi hiyo kwa muda wa miaka
nane.
Akitangaza matoke hayo Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Ali Aboth, ambaye
pia ndie msimamizi wa uchaguzi huo akitangaza matokeo hayo, amemtangaza Edwin
Soko kuwa Mwenyekiti mpya wa Misa -Tan kwa kupata kura 33, akifuatiwa na Said
Mmanga aliyepata kura 9 na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Betty Masanja
aliyepata kura 3 wakati kura moja ikiharibika.
Katika uchaguzi huo jumla ya wajumbe waliopiga kura walikuwa 46 na viongozi waliochaguliwa wataongoza taasisi hiyo nyeti ya vyombo vya habari na waandishi wa habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Muandishi: Mussa Mkilanya.
0 Comments