Katika kuadhimisha miaka 63 ya
Uhuru wa Tanganyika leo Halmashauri ya mji Kasulu imetekeleza agizo la Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kufanya
maadhimisho hayo kwenye maeneo ya kijamii.
Akizungumzia maadhimisho hayo
mkurugenzi wa Halmashari mji Kasulu Mwl. Vumilia Simbeye amesema lengo la
kufanya usafi katika Hospitali hiyo ni kuhakikisha mazingira ya hospitali yanakuwa safi .
Mwl. Simbeye ameelekeza watendaji
wa kata na mitaa kuhakikisha wanafuatilia hali ya usafi wa mazingira katika
maeneo yao.
Kwa upande wake Katibu Tawala
wilaya Kasulu Bi,Theresa Mtewele amewasisitiza wananchi kuwa wazalendo kwa
kushiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira.
Mkuu wa Jeshi la polisi Wilaya ya
Kasulu SSP Sango amesema jeshi la polisi
litaendelea na zoezi la usafi ili na
kuhakikisha vichaka vyote vinavyotumiwa na wahalifu vinafyekwa.
Aidha SSP Sango amesema suala la
usafi ni jukumu la kila mmoja bila kujali siku za maadhimisho,
huku akiwataka wananchi kufichua wahalifu ili kuendelea kudumisha Amani na
Utulivu ulioachwa na muhasisi wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.
Haya ni maadhimisho ya miaka 63 ya
uhuru wa Tanganyika huadhimishwa December 9 ya kila mwaka.
Mwandishi:Ellukaga Kyusa
Mhariri:Harieth Dominick.
0 Comments