Hayo yamebainishwa Watu
wanaoishi na VVU katika kambi ya wakimbizi ya Nduta wakati wa maadhimisho ya
siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika jana katika kambi ya wakimbizi wa Burundi
ya Nduta ikiyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma
Mmoja wa watu wanaoishi
na virusi vya Ukimwi kwa miaka 13 ambaye hakutaka majina yake yatajwe amebainisha
kuwa wamekuwa wakiitwa majina mabaya
yanayokatisha tamaa ya kuishi.
"Wanadiriki kutuita
tumeoza ,wafu na maneno mengi ya udharirishaji licha ya kwamba sisi hatuna
shida tunajua hali zetu na tunaweza kufanya kila kitu “alisema Mama huyo mwenye
watoto 4 wasiyo na maambukizi
Kwa upande Bakuru Ephraim
ambaye pia ameishi na VVU Kwa miaka 16 anasema kutokujitambua kwa baadhi ya watu
ndiyo chanzo Cha unyanyapaa Kwa watu wanaoishi na VVU.
"Kama unavyoniona
huwezi jua kama Nina Virusi vya Ukimwi na anafanya kila kitu na Nina watoto
saba wote hawana Ukimwi hata Mke wangu hana maambukizi ya VVU Kwa sababu
tunafuata maelekezo ya Wataalam wa Afya " Alisema Bukuru
Bukuru ambaye ni mkimbizi wa Burundi anabainisha kuwa Watu wajue Virusi vya Ukimwi ni kama Magonjwa mengine ya moyo, Kansa,Kisukari ambayo watu wanaishi nayo maisha yao yote wakizingatia maelekezo ya madaktari
“Tunapongeza na kushukuru
Mashirika yanayohudumia wakimbizi chini ya UNHCR hususani taasisi ya Timu za
Afya ya Kimataifa (Medical Teams International –MTI) kwa namna wanavyotoa
huduma mbalimbali za afya kwa wakimbizi na usaidizi wa kiafya na kijamii kwa
watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, bila MTI maisha yetu yangekuwa hatarini”
Alisisitiza Bw. Bukuru
Katika Maadhimisho hayo ambayo yaliunganishwa pamoja na siku ya
Ukimwi duniani ikiratibiwa na shirika la timu za afya kimataifa (MTI) na Baraza
la wakimbizi la Denmark (DRC) imebainishwa kuwa watu wenye ulemavu na wanaoishi
na virusi vya UKIMWI husahaulika katika vipaumbele vya utoaji wa huduma.
Inaelezwa kuwa jamii ya wakimbizi wenye virusi vya ukimwi na wenye ulemavu wamekuwa wakisahaulika wakati wa utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo ulinzi.
Bw. Chongera Elias raia wa Burundi akisoma risala kwa niaba ya watu wenye ulemavu katika maadhimisho hayo Kambi ya Nduta.
“Sisi tunaoishi na ulemavu tunakabiliwa na shida nyingi, licha
ya kwamba tunapata misaada wakati mwingine tunahitaji usaidizi Zaidi mfano
wakati wa kusafirisha vyakula kutoka kituo cha ugawaji hadi majumbani na hata
wakati wa kurejea nyumbani kwa wanaohiyari kufanya hivyo, unajua sisi watu
wenye ukemavu inapotokea vita au machafuko yoyote sisi ni wahanga Zaidi na
wanapaswa kulindwa hata ukimbizini. Alisisitiza Bw. Chongera mwenye ulemavu wa
viungo.
Kwa upande wake Mratibu wa Elimu Kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI Kutoka shirika la Medical Team International (TMI) Calen Amos amesema maadhimisho hayo wameyaunganisha na siku ya walemavu duniani ili kuwapaelimu watu wenyelemavu kuhusu maambukizi ya VVU kwa kuwa ni kundi linaloguswa pia na maambukizi ya hayo.
"Tumeamua
kushirikiana na mashirika Mengine ikiwemo DRC kuunganisha na siku ya walevu Kwa
sababu ni miongoni mwa kundi ambalo halina Elimu na tunataka na wao wapate
Elimu maana pia wako watu wenye ulemavu wanaoishi na maambukizi VVU"
Amesema Kalen.
Calen amesema katika
kampeni za kuelekea siku hiyo walipima watu zaidi ya 700 na wakabaini watu 2
wenye maambukizi, huku jumla ya watu 360 katika Kambi hiyo wanaishi na
maambukizi, wanawake 222 na Wanaume 138.
"Hawa watu wawili
tuliowagundua wameisha ingizwa katika mfumo wa kupata Dawa (ARVs) na
wanaendelea na maisha Yao na tuna wenza 27 ambao Mmoja anamaambukizi na
Mwingine hana maambukizi na wanaishi vizuri na kupata watoto bila shaka
yoyote" anasema Calen .
Dkt. Godlove Kanyonga
kutoka MTI kitengo Cha Afya ya akili na Utengemao amekiri kuwepo Kwa Unyanyapaa
Kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU jambo linalowapa msongo wa mawazo
waathiriwa hao.
Wakimbizi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI katika kambi ya Nduta,wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wakiwa katika maadhisho ya siku ya UKIMWI Kambini hapo.
" Unyanyapaa upo wa
aina mbili Kwa muhusika na wa jamii,Muhusika asipojikubali na ali aliyonayo
anajinyanyapaa hivyo anapata msongo wa mawazo ,Lakini upande wa pili jamii
ikiwanyanyapaa hawa watu wanapata pia msongo wa mawazo (sonona ) wanafikia hata
Hatua ya kufanya maamuzi yasiyo sahihi" amesema Dkt Kanyonga.
Kutokana na hali hiyo
wizara ya mambo ya ndani idara ya wakimbizi ofisi ya mkuu wa kambi ya wakimbizi
ya Nduta imetoa wito kwa Mashirika yote yanayohudumia wakimbizi kurejea mipango
yake ya huduma kwa wakimbizi wenye mahitaji maalumu
Rai
hiyo imetolewa na Bw. Iddy Omary Mahuna ambaye ni afisa afya ya jamii kutoka
katika ofisi ya mkuu wa kabi ya wakimbizi ya Nduta akielekeza Mashirika
kupunguza bajeti za machapisho hususani fulana na kofia wakati wa maadhimisho
mbalimbali na pesa hizo zitumike kuwapa huduma walemavu na wenye virusi vya
Ukimwi
Kaimu Mganga mkuu wa
Wilaya Dkt Frederick Kilindo aliyekuwa mgeni rasmi akijibu Risala ya watu
wanaoshina virusi vya UKIMWI amesema mtu anayefanya unyanyapaa kwa Mtu
anayeishi na VVU akibainika anaweza kufungwa jela mwa Mmoja au kupigwa faini.
"Kwa mujibu wa Sheria
ya UKIMWI ya mwaka 2008 ukimnyanyapaa mtu mwenye UKIMWI unaweza kupigwa faini
ya Shilingi Milioni 2 au Kifungo Cha mwaka 1 jela na nadhani tutekeleze hii
Sheria" ansema Dkt Kilindo.
Baadhi ya Wakimbizi
walioshiriki sherehe hizo akiwemo Mhera Kolonari, amesema wamefurahishwa na
siku hiyo Kwani wamepata Elimu kuhusu UKIMWI na kupima bure.
Mwandishi: Harieth Dominick
Mhariri:Prosper Kwigize
0 Comments