Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa huu yafanyike katika ngazi ya Mikoa na fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe kwenye kutoa huduma za kijamii.
Amesema
hayo leo Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha Mawaziri kilichofanyika Jijini
Dodoma na kuongeza kuwa sherehe za Mwaka huu hazitahusisha Gwaride na Shughuli za
Kitaifa.
Mhe. Majaliwa amesema kila Mkoa unapaswa kuhakikisha kuwa Wilaya
zilizopo katika Mkoa husika zinafanya shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti,
usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama vile Kambi za wazee, Masoko,
Hospitali, mashindano ya michezo, makongamano na midahalo ya maendeleo.
Aidha amewataka wananchi kushiriki
katika shughuli hizo ili kuwa sehemu ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi
cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania.
“Naagiza Wakuu wote wa
Mikoa ya Tanzania Bara, kufuata ipasavyo maelekezo yaliyotolewa na Serikali ili
kuhakikisha Maadhimisho hayo yanafanyika kwa kama ilivyo tarajiwa,” amesema
Mhe. Majaliwa.
Waziriki Mkuu Mhe. Majaliwa
amesema shughuli za Maadhimisho ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa Mwaka
huu zilishaanza tangu mwanzo wa mwezi Disemba, na kilele ni Desemba, 09 mwaka
huu.
Muandishi : Mussa Mkilanya.
0 Comments