Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awaachia huru Wafungwa 1548

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza msamaha kwa Wafungwa 1548 ambapo Wafungwa 22 kati yao wameachiliwa huru  na Wafungwa 1526 wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huo leo.

 Taarifa iliyotolewa leo na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dodoma imesema msamaha huo wa Rais Samia ni sehemu ya kuadhimisha Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

 Aidha Mhe.Dkt Samia amesema anatarajia Wafungwa walioachiliwa huru leo watarejea tena katika Jamii kushirikiana na Wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa,huku akiwataka kujiepusha  kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

 

Post a Comment

0 Comments