RAIS MWINYI ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya  Heshima ya Uzamivu  ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Chuo Kikuu cha Zanzibar kimemtunuku  Shahada hiyo ikiwa ni kutambua   na kuthamini Mchango  wa Uongozi wake  Unaoacha Alama  na historia itakayokumbukwa  wakati wote.

 Hafla ya kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika leo tarehe 5 Disemba 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa mwaka 2024

 Shahada hiyo ya Heshima ya Uchumi  ametunukiwa kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan  Ukuaji wa Uchumi    na Maendeleo yaliopatikana Kipindi kifupi cha Uongozi wake wa miaka minne  akiwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

 Rais Dkt. Mwinyi amekishukuru Chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa ajili ya Maendeleo ya nchi.

 Aidha Rais Dkt.Mwinyi  amebainisha kuwa  Shahada hiyo aliotunukiwa Inaakisi kazi nzuri inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya kufanya  Maendeleo zaidi.

Na Mwandishi wetu.

 

 

Post a Comment

0 Comments