Timu ya wananchi Yanga SC kutupa karata yao ya pili michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika kesho dhidi ya Algers ya Algeria majira ya saa nne kamili usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Kupitia kwa Afisa habari wa timu hiyo Ally Shaaban Kamwe amesema kuwa majeruhi wameanza mazoezi na ikimpendeza kocha watatumika kutetea nenmbo ya klabu Yao.
"Majeruhi wameanza mazoezi kama halid Aucho,Diara na wengine kwa hiyo ni waombe mashabiki na wadau wa soka muiyombee timu yetu,benchi la ufundi ili kesho tuamke wenye afya tele tayari kuvuna alama tatu hapahapa kwao Algeria"Amesema Kamwe.
Nahodha msaidizi wa timu hiyo Dickson Job amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mapambano hasa ipo ya kutosha na wanahitaji matokeo chanya ugenini.
"Kila mchezaji anajituma ili kupata nafasi ya kuitetea nembo ya klabu yetu kwa hivyo sisi tupo tayari kutekeleza maagizo ya kocha kwa lengo Moja tuu kupata matokeo"Amesema Job.
Nao wadau wa soka kutoka Kasulu Mkoani Kigoma wamesema kuwa kikosi kilichosafiri wanamatumaini kuwa watapata matokeo mazuri wakijituma na kutekeleza kili walichoagizwa na kocha kufanya uwanjani.
"tunajua kuwa wameanza vibaya michuano ya klabu bingwa lakini sio sababu ya kukata tamaa kwamba hawawezi kuvuna alama tatu ugenini kikubwa wajitume na wasitie woga wacheze kwa nidhamu yote yanawezekana"Wamesema wadau wa soka.
Yanga SC wanahitaji alama tatu Ili kujiweka nafasi nzuri katika kundi lao ambao nitimu pekee iliyoruhusu nyavu zake kutikiswa na kupoteza alama tatu uwanja wa nyumbani kwa kufungwa magoli mawili(2) dhidi ya Al hilal ya Sudan.
Mwandishi:Eunice Jacob
Mhariri: Harieth Dominick
0 Comments