Akizungumza Decemba 11 katika kikao cha baraza la madiwani la
halmshauri ya mji Kasulu Kanalii Mwakisu ametoa maagizo kwa mkurugenzi na afisa
elimu wa halmashauri hiyo kuhakikisha wanafuatilia na kubaini sababu za kiwango
cha Elimu kushuka katika halmshauri hiyo.
“Sasa hivi tumekuwa wa 6 mimi sijaridhishwa na usimamizi wa shule
za msingi na matokeo yanavyotokea Afisa elimu sijaridhika na mwenendo wa ufaulu
wa idara yako nimefanya utafiti miaka mitatu nyuma kila muda mnashuka viwango
nitaanza ukaguzi wa kushtukiza, mkurugenzi nataka uniambie kila shule ina
walimu wangapi haiwezekani kila mwaka mnashuka tu hadi mmeshika nafasi ya 6
haiwezekani” Amesema Kanali Mwakisu.
Aidha makamu mwenyekiti wa
halmshauri ya mji kasulu bw.Selemani Kwirusha ameeleza kusikitishwa na matokeo
ya darasa la 7 na kuwataka madiwani kushirikiana katika kukuza taaluma ya
wanafunzi shule za msingi katika halmashauri ya Mji Kasulu.
“Nimeyapokea Matokeo haya
kwa masikitiko makubwa, hiki alichokisema mkuu wetu wa wilaya hakijafurahisha
mtu yeyote na waheshimiwa Madiwani niwaombe sana kila mtu alichukulie kwa uzito
swala hili ni aibu pamoja na mkurugenzi nimuagize kwa umuhimu huu ambavyo
umeuchukulia kwa jinsi mlivyojipanga na kabineti yako mje na visababishi ili tujuwe sababu ni nini”
Amesema makamu mwenyekiti wa halmshauri Kwirusha.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi
wa halmshauri ya mji kasulu Mwl Vumilia Simbeye amesema wameshaanza ufuatiliaji
na kutoa maagizo kwa wakuu wote wa shule za msingi kuhakikisha wanasimamia
swala hili ili jitihada za kukuza taaluma ya elimu kwa shule za msingi.
“Matokeo mazuri sisi ndo
tutakaosababisha na matokeo mabaya sisi ndo tutasababisha hatuna namna ya
kukwepa, kwa kuwa sis indo wasababishi wa matokeo hayo tayari tushafanya tathmini
na tumejiona tulipo hakuna ambaye ameridhika na tumeshaanza mikakati ya
kuboresha na tunaamini mwakani tutafanya kitu bora tofauti na mwaka huu.
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma
iling’ara katika matokeo ya darasa la saba 2024 kwa kushika nafasi ya pili
kimkoa kati halmashauri nane zilizopo baada ya kupata ufaulu wa 85.6%.
Mhariri, Ramadhani Zaidy
0 Comments