Mkurugenzi msimamizi wa mpango wa usimamizi wa watu wenye Ulemavu Tanzania (DMP.T) Subira Mkumule amewataka Walemavu wasisitizwa kudai haki zao za msingi kwa kufuata sheria bila kuogopa.
Ameyasema haya leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wakati wa kongamaano la siku ya ulemavu Dunia na kuongeza kuwa walemavu hawapaswi kuwa waoga katika kupambania haki zao.
Amesema kundi la walemavu linapaswa kupewa kipaumbele katika elimu kwani visababishi vya ulemevu ni vingi ikiwemo magonjwa ya kuambukiza yanaweza kusababisha ulemavu kwa watoto waliopo tumboni kabla ya kuzaliwa.
“Magonjwa ya kuambukiza yanaweza kusababisha ulemavu
kwa mototo ambaye bado hajazaliwa lakini pia ulemavu unaweza kutokea wakati
mama anajifungua kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinaweza kutokea wakati
anajifungua pia
ajali ni miongoni chanzo cha ulemavu,” amesema Mkumule.
Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kiganamo Dkt. Moshi Kigwinya akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Aidha kwa upande wake Dkt. Moshi Kigwinya ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kiganamo amewaeleza walemavu namna wanavyopaswa kufuata utaratibu ili kupata huduma ya matibabu mapema tofauti na watu wengine.
“Ni utaratibu ambao umeweka na miongoni mwenu wapo
wanaofahamu, sera ya serikali inayosema mlemavu anapaswa apewe kipaumbele
katika huduma zote hivyo mkifika kituo chochote cha afya wambieni mimi napaswa
kuhudumiwa” amesema Dkt. Kigwinya.
Dkt. Kigwinya ameongeza kuwa walemavu ambao hawawezi
kuchangia huduma za afya kuna utaratibu madhubuti wa kufuata na kupewa fomu ya msamaha
kwa kupitia ofisi ya Ustawi wa jamii ili kuingia katika kipengere cha msamaha.
“Walemavu wengi huwa hawana uwezo wa kuchangia huduma
za Afya na Serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia walemavu ambao hawana uwezo
wa kuchangia huduma wanapitia kwa Usitawi wa jamii ili kupata fomu ya msamaha
wa huduma
ya malipo” amesema Dkt. Kigwinya.
Watu wenye ulemavu wakiwa kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya ulemavu Duniani katika ukumbi wa Halmashauri ya Kasulu Mji.
Katika hatua nyingine Afisa Utamaduni wa Jamii Katika
Halmashauri ya Mji Kasulu Ndg. Salum Massagah. amesema Ofisi yao imeweka
mkakati kuhakikisha inawasaidia walemavu kupata elimu wakiwa katika umri mdogo
na kuwapatia vifaa vyote vya kusomea kwa wenye uhitaji huo.
“kwenye upande wa elimu tumehakikisha tunaboresha
miundombinu rafiki pale atakapokuwa shule pia tunasisitizwa kuwapa huduma ya
elimu wakiwa umri mdogo ili kuwasaidia kuwapunguzia hali hiyo ya ulemavu lakini
pia kuwapatia
vifaa vinavyohitajika wakati akiwa shuleni,” amesema Massagah.
Kwa upande wake Zakayo Nkohozi amabaye ni Mwenyekiti
wa Shirikisho la watu wenye Ulemavu Wilaya Ya Kasulu (SHIVYAWATA), amezungumza
kwa niaba ya walemavu ameseama mafunzo yaliyotolewa na wataalamu yanawasaidia
kutambua haki zao za msingi.
Ifahamike kuwa siku ya ulemavu dunia huadhimishwa kila
inapofika Disemba 3 kila mwaka, Kwa Wilaya ya Kasulu kongamano la kuadhimisha
siku ya walemavu limefanyika katika Halmashauri ya Kasulu Mji na kuhudhuriwa na
viongozi
mbalimbali pamoja na walemavu wa aina yote.
Mwandishi: Sharifat Shinji
Mhariri: Mussa Mkilanya
0 Comments