Jashi la Polisi Kanda maalum ya Dar es saalam limesema kuwa linawashikilia watu nane wanaotuhumiwa kwa zoezi la utekaji wa Ndg. Deugratius Tarimo Mkazi wa Kibaha Mailmoja Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na jeshi Kanda
Maalum ya Dar es salaam leo imemnukuu Kamanda Jumanne Muliro kuwa Jeshi la
Polisi limewakamata watuhumiwa nane wa tukio la utekaji wa Ndg. Deogratius Tarimo
katika eneo Kiluvya jijini Dar es salaam.
Kamanda Muliro, ameongeza kuwa watu hao wamekamatwa kwa
nyakati tofauti tofauti, huku gari aina ya Toyota Raum ambayo ilitumiwa wakati
wa utekaji imekamatwa ikiwa na namba ambazo si halisi T 237 EGE na baada ya
ufuatiliaji imebainika kuwa namba halisi ya gari hiyo ni T237 ECF.
0 Comments