Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, ametangaza nia yake ya kugombea tena ubunge
wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 huku akiwaonya watu aliowaita
wanafiki.
Akizungumza Jumatano Januari 1, 2025 katika hafla ya Fungua Day, ameweka
wazi msimamo wake dhidi ya watu wanaojifanya kumuunga mkono huku wakishirikiana
na wapinzani wake kisiasa.
“Hakuna boya hata moja kwangu, nawaambia wapigakura wangu msidhani kwamba nyoka
mdogo hana sumu. Sumu ni ileile, haijalishi ukubwa wa nyoka,” amesema Profesa
Mkumbo.
Akionyesha dhamira yake ya kuendelea kutumikia wananchi wa Ubungo, Profesa
Mkumbo amesema: “Mungu akijalia afya njema, nitagombea tena 2025. Nimejipanga
zaidi ya 2020, na siasa si mahali pa kuhubiri mbinguni. Katika siasa unambeba
anayekubeba, anayekutupa unamtupa,” amesema.
Na mwandishi wetu
Mhariri:Abel Mahenge
0 Comments