Tukio hilo limetokea Jumatano Januari 1, 2025 wakati ng’ombe hao wakichungwa
katika hifadhi ya Kalambo mkoani humo, huku mmiliki mpaka sasa akiwa
hajafahamika.
Mhifadhi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Ibrahim Mkiwa amesema wamewakuta ng’ombe
hao wamekufa hifadhini humo, huku akitoa rai kwa wananchi kutoingiza mifugo
hifadhini.
Mganga Mkuu wa mifugo wilayani humo, Dk Ennosy Luvinga amesema baada ya
uchunguzi wamebaini ng’ombe hao wamekufa kwa kupigwa na radi.
Hili ni tukio la pili mfululizo kwa mifugo kufa kwa kupigwa na radi mkoani
humo, ambapo la kwanza lilitokea Desemba 9, 2024 baada ya ng'ombe 22 kupigwa
radi wakiwa zizini katika Kijiji cha Songambele Kata ya Azimio wilayani
Sumbawanga.
Na mwandishi wetu
Mhariri : Abel Mahenge
0 Comments