Ufaulu matokeo kidato cha nne waongezeka kwa asilimia 3%

 

 



Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa kidato cha nne na kusema ufaulu umeongezeka kwa asiliimia 3 na kufikia asilimia 92.37 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2023.

Matokeo hayo yametangazwa leo Alhamisi na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said Mohammed jijini DaresSalaam ambapo Jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 92.37 wamefaulu ambapo wamepata madaraja ya I, II, III na IV.

Said, umeongezeka kwa kusema  Ubora wa ufaulu wa Madaraja ya Kwanza mpaka tatu ni mzuri zaidi kwa kundi la wavulana, ikilinganishwa na Wasichana, ambapo Wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 48.90 ya Wavulana wote, huku Wasichana wakiwa 102,084 sawa na asilimia 37.59 ya Wasichana wote

"Matokeo ya kidato cha nne 2024 takwimu zinaonyesha kuwa ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 3, na hivyo kufikia asilimia 92.37 ambapo watahiniwa laki nne sabini na saba elfu mia mbili sitini na mbili, kati ya watahiniwa laki tano kumi na sita elfu mia sita tisini na tano, kwenye matokeo wamefaulu kwa kupata madaraja ya kwanza, pili, tatu na nne."

Pia Baraza hilo la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo ya wanafunzi 67 waliofanya udanganyifu na wanafunzi 5 walioandika matusi kwenye karatasi za kujibia huku  likizuia matokeo ya wanafunzi 459 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote zikiwemo matatizo ya kiafya na baraza liokitoa nafasi ya kurudia mitihani kwawanafunzi hao mwaka 2025


Mwandishi wetu.

Mhariri  Paul Masanja 



Post a Comment

0 Comments