Wakimbizi 5000 Nyarugusu wanufaika na Misaada kutoka Itel Tanzania.



Takiribani Wakimbizi 5000 kati ya 135,000 waliopo katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamenufaika na Misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya milioni 100 kutoka Kampuni ya Itel Tanzania kwa kushirikiana na shirika la wakimbizi duniani UNHCR

Misaada hiyo imetolewa Leo na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Itel Tanzania Bi. Sophia Almeida Mafiri na kukabidhi kwa mkuu wa kambi hiyo Ndg.Siasa Manjenje, na kusema wamekabidhi misaada ya vitu hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.

“Sisi kama Itel Tanzania tumeungana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa ajili ya kuleta Misaada kwa wakimbizi hapa Nyarugusu na misaada ambayo tumeitoa leo ni Pisi 5000 ya vyandarua, Vitenge, Kanga, taulo za kike na nguo za ndani za watoto, wanawake na wanaume vyenye Thamani ya zaidi ya million 100” Amesema Bi, Sophia Almeida.

Meneja Masoko kutoka kampuni ya Itel Tanzania Bi. Sophia Almeida Mafiri akisoma hotuba wakati wa kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali katika kambi ya Wakimbizi Nyarugusu.

Katikati ni Mkuu wa kambi ya Wakimbizi Nyarugusu 
Ndg. Siasa Manjenje  na kushoto ni Mkuu wa shirika la wakimbizi (UNHCR) Wilaya Kasulu Bw. Jean Bosco wakipokea  Vitenge kutoka kwa Meneja Masoko kutoka kampuni ya Itel Tanzania Bi. Sophia Almeida Mafiri

Aidha kwa Upande wake Mkuu wa shirika la wakimbizi (UNHCR) Wilaya Kasulu Bw. Jean Bosco amewashukuru Itel kwa misaada ya waliyoitowa na kuwaomba waenendelea kutoa misaada kila wanapopata nafasi huku akibainisha shirika la (UNHCR) linapitia changamoto za kifedha ambapo imekuwa ngumu kuisaidia serikali kutatua changamoto kwa wakimbizi.

“Kwanza niwashukuru Itel kwa kutupa sapoti ambayo wameitoa kwetu na ni kweli taasisi yetu inapitia changamoto za kifedha hivyo imetufanya tushindwe kuisaidia serikali ya Tanzania katika kuwasaidia wakimbizi waliopo Tanzanzania hivyo kilio cha wakimbizi sasa kimesikika na Itel wameweza kusaidia hivyo Itel asanteni sana na karibuni tena” Amesema Bw. Jean.

Mkuu wa shirika la wakimbizi (UNHCR) Wilaya Kasulu Bw. Jean Bosco

Katika hatua nyingine mkuu wa Kambi Ndg. Siasa Manjenje amesema misaada hiyo itasaidia wakimbizi waliopo katika kambi hiyo kulingana na Idadi ya vitu walivyopokea kutoka Itel Tanzania huku akitoa wito kwa mashirika mengine kujitokeza kusaidia wakimbizi waliopo Nyarugusu.

“Tunawashukuru Itel kwa misaada waliyoitowa kwani itaenda kusaidia watu wengi maana katika kambi kuna watu wengi wenye uhitaji hivyo natowa wito kwa mashirika mengine ya kiserikali na mashirika ya watu binafis pamoja na watu wengine tunawakaribisha sana Nyarugusu”Amesema Manjenje.

Mkuu wa Kambi ya wakimbizi Nyarugusu  Ndg. Siasa Manjenje akizungumza mbele ya hadhara ya umma wa wakimbizi wa Nyarugusu.

Kwa upande mwenyekiti wa Kambi ya wakimbizi Nyarugusu Ndg. Manelakiza Japhet ameshukuru kwa msaada uliotolewa huku akikiri uwepo wa mahitaji kwa wakimbizi waliopo katika kambi ya Nyarugusu na kuomba mashirika mengine kujitoa kwa ajiri ya wakimbizi.

“Ni ukweli usiopingika kwa sasa shirika la (UNHCR) linachangamoto ya kifedha ambayo inapelekea lishindwe kutoa misaada hivyo tunaomba mashirika mengine yatusaidie kwani kambini kuna mahitaji mengi yanayohitajika leo ni Itel ambao wametuletea misaada tunawashukuru sana kwa misaada ambayo leo mmeitoa” Amesema Mwenyekiti Manelakiza.


   Mwenyekiti kambi ya wakimbinzi nyarugusu pamoja na baadhi ya wakimbizi baada           yakupokea zawadi kutoka itel

Nao baadhi ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu akiwemo Zabibu Bwenge na Bokeka Matumaini wamefurahishwa na maamuzi ya Itel Tanzania kwa kuwaletea misaada huku wakiwasisitiza wadau wengine kuwaletea misaada ambayo itawasaidia wakimbizi katika mahitaji mbalimbali.

Baadhi ya wakimbizi wa kambi ya Nyarugusu wakiwa katika Hafla ya ugawaji misaada kutoka kampuni la Itel Tanzania.

Baadhi ya mizigo waliyopatiwa wakimbizi Kambi ya Nyarugusuusu ikiwa kwenye Lori la Mizigo

Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu inahudumia takiribani wakimbizi 135,000 kutoka Mataifa saba, kutokana na changamoto za kifedha kwa shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani (UNHCR) wadau na mashirika mbalimbali wanaombwa kusaidia mahitaji katika kambi zilizopo katika mkoa wa Kigoma.

Mwandishi; Sharifat Shinji

Mhariri; Lutakilwa Lutobeka 




Post a Comment

0 Comments