Wanufaika watakiwa kurejesha fedha za mikopo kwa wakati


Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kasulu na diwani wa kata ya heru juu Noel Hanula na mgeni rasmi amewataka wanawake ambao ni wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 ya pato la halmashauri kutumia fedha hizo kwa ajili ya maendeleo na sio mambo binafsi.

Mh Noel Hanula amesema hayo leo januari 22, 2025 katika ukumbi wa halmashauri ya mji kasulu wakati wakikabidhi pesa hizo za mikopo kwa wanawake hao na kusema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha mkopo huo unatumiwa katika malengo yaliotumika kuomba mkopo huo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kasulu na diwani wa kata ya heru juu Noel Hanula na mgeni rasmi akihutubia wanufaika wa mikopo ya halmashauri.

“mikopo hii umetolewa na mh Rais kwa lengo la kujikwamua kiuchumi kwa kuwa awali ilisitishwa kutokana na wanifaika kutumia kinyume na malengo hivyo niwaombe mama zangu tutumie mikopo hii kwa lengo la kujikwamua kiuchumi kama dhamira ya Rais Samia na kutumia kwa matumizi yetu binafsi” amesema Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kasulu na diwani wa kata ya heru juu Noel Hanula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Mji Mwalimu Vumilia Simbeye amewasisitiza wanawake hao kuhakikisha wananza marejesho ya mikopo hiyo kwa wakati kama walivyokubaliana ili kuepusha usumbufu kwa serikali kwani riba imeondolewa kwa lengo la kurahusisha ulipaji wa mikopo hiyo.

 Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Mji Mwalimu Vumilia Simbeye akihutubia wanufaika wa mikopo ya halmashauri

“wananchi wote inabidi watambue kwamba mikopo hii haina riba na ni nafuu kwa wananchi wa wananufaika hivyo basi nitoe wito kwa wananchi waliochukua mikopo hii kurudisha katika muda ulipangwa ili na wengine wanufaike kwa sababu tumeona haja ya kutoa riba katika mikopo hii ili urejeshwaji wake uwe rahisi kwao” amesema Mkurugenzi wa halmashauri ya Kasulu Mji Mwalimu Vumilia Simbeye.

Nao baadhi wanufaika wa mikopo kutoka katika vikundi mbalimbali ambavyo leo vimepata mikopo hiyo wameahidi kutekeleza kule kilichoainishwa katika makubaliano ya awali kabla kuchukua mikopo hiyo kwa ajili ya kuinua uchumu kwa kundi husika na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.


Baadhi ya wanufaika wa mikopo ya halmashauri 
“ sisi kwetu tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga kabla ya kuchukua mikopo hiyo lakini pia tumejiopanga kurejesha pesa hizo kwa wakati na tumalize salama ili tuendelee kunufaika na hii mikopo” wamesema baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo.

Moja ya kikundi kilichonufaika na mikopo hiyo katika picha ya pamoja na uongozi wa halmashauri wakikabidhiwa mfano wa cheki ya malipo

Halmashauri ya mji kasulu imetoa mkopo wa Zaidi ya shilingi milioni 34 la laki sita ikiwa ni asilimia 10 ya pato la halmashauri hiyo huku fedha hizo zikienda katika makundi 5 ya wanawake katika halmashauri hiyo.

Mwandishi: Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments