Kampeini ya msaada wa kisheria ya Samia legal aid imefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa mwaka Moja katika kata ya kulugongo
Mgogoro huo uliokuwa ukilalamikiwa na bi Angelina Kadakila kuhusu ardhi iliyouzwa na mme wake Yassin Jonas bila kumshirikisha mke wake kwa Debora Danford ambae amekubali kulipa fidia ya garama ya lakisita
Mara Baada ya kupatika a suluhu hio wananchi hao wameshukuru ujio wa msaada huo wa kisheria kwani umewaepusha kutumia garama nyingi kwenda kutafuta haki na na kuepusha mgogoro baina Yao
Mratibu wa kampeini hio ya msaada wa kisheria halmashauri ya wilaya kasulu Moses basila amesema katika kata ya kulugongo wamebaini uwepo wa migogoro mingi ya ndoa inayopelekea kujimilikisha Mali na ukatili wa kijinsia unaopelekea kukosekana kwa malezi ya watoto
Ameongeza kuwa kupitia msaada huo wa kisheria wa Samia legal aid lengo kubwa ni kutatua changamoto za migogoro na kufikia makubaliano kwa njia ya majadiliano kama ilivyofanyika kwa bi Angelina na Debora
Mwandishi: Paul Masanja, Buha News
0 Comments