Mkuu wa wilaya ya Tarime mhe Mejaa Edward Frowin Gowele amelipongeza kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Talanta iliyopo kata ya Nyandoto iliyopo halmashauri ya mji Tarime.
Ametoa pongezi hizo leo Februari 19,2025 wakati wa ziara yake fupi katika shule hiyo na kiwapongeza waumini wa kanisa hilo na uongozi kwa kutambua uhitaji wa jamii katika kuimarisha sekta ya elimu.
Aidha amewataka waumini katika makanisa mbalimbali kwa kushirikiana na jamii Kuimarisha amani na ulinzi pia kushirikiana na serikali pale ambapo makanisa hayo yatahitaji ushirikiano huo.
Kwa upande wao viongozi wa Kanisa hilo wameishukuru serikali kwa ushirikiano baina yake na madhehebu na kuahidi kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo
Mwandishi: Paulina Majaliwa
0 Comments