Pongezi hizo zimetolewa Februari 27, 2025 jijini
Dodoma wakati wa hafla ya kufunga rasmi Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme
kutoka Makambako hadi Songea, uliofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa
kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
Mhandisi Mramba amesema kuwa mradi huo wa njia
ya umeme kutoka Makambako hadi Songea umehusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha
umeme yenye msongo wa kilovoti 220 kwa urefu wa kilomita 245, ujenzi wa vituo
vya umeme vya Madaba na Songea mjini, upanuzi wa kituo cha umeme cha Makambako
pamoja na kusambaza umeme katika vijiji 120.
“Tunaipongeza Serikali ya Sweden kwa mchango
mkubwa ambao wanatusaidia katika kufadhili miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo
kupeleka umeme vijijini hapa nchini.” Amesema Mramba
Amesema kuwa, Serikali ya Sweden imetoa mchango
mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini iliyotekelezwa katika
maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya za Urambo, Serengeti, Simanjiro na
Ukerewe, pia Sweden ndio nchi ya kwanza kusaidia miradi ya umeme vijijini hapa
nchini.
Miradi mingine iliyofadhiliwa na Sweden ni mradi
wa ujenzi wa Bwawa la Mtera na Kidatu.
Ameongeza kuwa, Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Sweden kwa sasa inaendeleza ukarabati wa kituo cha kuzalisha
umeme cha Hale ambacho ni cha muda mrefu ambacho kitazalisha megawati 21
baada ya ukarabati kukamilika.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe.
Charlotta Ozaki Macias ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la
umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kusimamia
kikamilifu utekelezaji wa miradi ya umeme.
Amesema mradi wa Makambako hadi Songea
uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka 20 kukamilika kwake kutaendelea kunufaisha
wananchi wengi katika upatikanaji wa huduma ya umeme hasa maeneo ya vijijini.
0 Comments