Mtandao wa Redio za kijamii Tanzania TADIO kwa ufadhili wa shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF wametoa mafunzo kwa vyombo vya kijamii ili kufahamu jinsi ya kuripoti habari za magonjwa ya mlipuko na masuala ya watoto kwenye jamii.
Mafunzo hayo yamemeendeshwa mjini Bukoba mkoani Kagera kuanzia tarehe 10 Hadi 12 februari 2025 ambapo takribani wawakilishi wa Redio za kijamii 13 wamehudhuria mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yametolewa mahususi kutokana na
uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Mkoa wa Kagea ambapo kwa pamoja
waandishi wa Habari, wahariri na waratibu wa vipindi radioni wameelimishwa juu
ya namna bora ya kuandika, kuripoti na kutangaza habari kwa kuzingatia kanuni
na taratibu za Wizara ya Afya na shirika la afya duniani WHO.
Miongoni mwa masomo yaliyofundishwa ni Pamoja na historia ya ugonjwa wa Marburg, dalili zake, madhara na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo pia wamefundishwa kuhusu jinsi ya kuandika habari za watoto na ukatiri wa wanawake ndani ya jamii.
Aidha walifundishwa jinsi ya kuandaa vipindi vyenye mvuto kwa jamii ambavyo vina utatuzi wa changamoto zao, namna ya kuandaa maswali ambayo yanatokana mapungufu au changamoto ambazo zipo ndani ya jamii ili kuleta uwajibikaji wa serikali na jamii kwa ujumla.
Mkufunzi kutoka chama cha waandishi wa Habari za vijijini ambaye pia ni mwakilishi wa shirika la utangazaji la Ujerumani DW Bw. Prosper Kwigize aliwaelekeza washiriki wa mafunzo namna kutambua vyanzo (influencers), Imani zilizopo ndani ya jamii (agreed realities) na matokeo yenye msisimko kwa jamii (emotions) ni pamoja, kufanya mazoezi ya uandaaji wa kampeni za afya kwa vitendo
Kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo, waandishi wa habari wamepata nafasi ya kufanya matembezi katika fukwe ya ziwa Victoria na kubaini tabia au matatizo ambayo wameyatumia kutengeneza swali mahususi ili kupata ufumbuzi kwa wahusika.
Pamoja na mambo mengine wamehimizwa kuancha kutengeneza habari za upotoshaji na badala yake wajikite kuandaa habari na vipindi ambavyo vina taarifa sahihi na zinazoleta matokeo chanya.
Mafunzo hayo kwa ujumla wake yametolewa na
Baptist John mwenyekiti wa TADIO Tanzania, Dkt. Salum kimbau kaimu Afisa afya
mkoa wa Kagera, Stanley
Magesa kwa niaba ya shirika la IPSOS, na Dkt
Chikondi Khangama kutoka UNICEF, na Mwandishi wa habari wa shirika la
utangazaji Ujerumani DW, Katibu mkuu wa RUJAT na Mwasisi wa TADIO Prosper Laurent
Kwigize
Mwandishi: Devotha Martine
0 Comments