Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia kwa wananfunzi ni Moja ya sababu kubwa inayowafanya kukatisha masomo
Hayo yameelezwa timu ya wataalamu wa kampeni ya Msaada wa kisheria ya Samia legal aids kampeni ilipozitembelea shule ya sekondari Rungwe mpya katika kata ya Rungwe mpya na shule ya msingi Bulanzwili kata ya Kulungongo
Afisa usitawi wa jamii ndani ya halmashauri ya wilaya kasulu bi Subira amewasihi wananfunzi kutoa taarifa juu ya ukatili mbalimbali ambao wanaweza kufanyiwa ikiwemo maeneo ya shuleni, mtaani, na majumbani
Kwa upande wake meatibu wa kampeni hio katika halmashauri ya wilaya kasulu wakili Moses Basila amewataka wananfunzi kutimiza wajibu wao lakini pia kuzitambua haki zao za msingi ili kuepukana na maku ndi
Ameongeza kwa kuwashauri wanafunzi kuwamini walimu wao katika utoaji wa taarifa kama watakunbana na matatizo ya ukatili mashuleni pamoja na majumbani
Mwandishi: Paul Masanja, Buha News
0 Comments