Maelfu ya Wakimbizi wa DRC waingia Burundi

Zaidi ya wakimbizi 47,000 wa Kongo wamepokelewa na UNHCR katika wilaya ya Rugombo, jimbo la Cibitoke, kuanzia tarehe 14 hadi Jumanne ya week hii

Kiongozi wa shirika UNHCR nchini Burundi alitoa tangazo hilo Ijumatano hii 26/02/2025. UNHCR, shirika la ustawi wa watoto UNICEF, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na wengine walikuwa wametembelea wakimbizi hao wakikongo Wakiandamana na wawakilishi wa Afrika Kusini na Tanzania nchini Burundi.



Brigitte Mukanga anasema wakimbizi hao wako kwenye uwanja wa soka shuleni na makanisani. Anasema kuna zaidi ya watoto 7,000 wengi wao wanadaiwa kukimbia bila wazazi. Pia anaripoti kuwa kuna zaidi ya wanawake 2,500 wajawazito na wanaonyonyesha ambao wanahitaji msaada. 

Brigitte Mukanga Eno amesema wakimbizi hao watawahamishiwa katika mikoa ya Rutana na Mwaro. Huku akiwaomba wale wote wanaoweza kusaidia kujitokeza ili kusaidia kwenye mahitaji ya wananchi hao.

Post a Comment

0 Comments