Breaking News! Rais Samia afanya uteuzi, DC atenguliwa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kuwapangia vituo Mabalozi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na kupangiwa vituo Mabalozi ni kama ifuatavyo:-

Bi. Rachel Stephen Kasanda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi. Bi. Kasanda anachukua nafasi ya Bw. Lauteri John Kanoni ambaye uteuzi wake umetenguliwa;

Prof. Jafari Ramadhani Kideghesho ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania;

CPA. Ashraph Yusuph Abdulkarim ameteuliwa kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo;

Balozi Hamad Khamis Hamad amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji; na

Balozi Mobhare Holmes Matinyi amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.


Post a Comment

0 Comments