Utafiti Tatuzi kuhusu Elimu Jumuishi wazinduliwa Kigoma,
Wananchi katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wameombwa kutojihusisha na vitendo vya Unyanyapaa kwa Watu wenye Ulemavu pamoja na kutojihusisha katika vitendo vya ukatili kwa watoto waliopo shuleni ili Kujenga usitawi na maendeleo bora katika jamii.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa wakati akizungumza katika Hafula ya Kongamano la uzinduzi wa program ya utafiti tatuzi kuhusu Usalama Jumuishi katika Elimu lililofanyika katika Kiwanja cha Mpira Kiganamo na kusisitiza jamii inawalinda watoto wote wenye ulemavu na wasio na ulemavu ili kujenga jamii bora.
“Naomba kila kiongozi wa Tanzania kuanzia ngazi za serikali za mitaa hadi ngazi ya taifa utendaji wake uanze kwa kuangalia ni kwa namna gani anasimamia kwa dhati usalama, ustawi na maendeleo ya watoto, kama wewe ni kiongozi wa kimila, kidini, kiselikali lazima uzingatie usalama, ustawi na maendeleo ya watoto” Amesema DKT. Mtahabwa.
Aidha Dkt. Mtahabwa amesema watu wote wanaojihusisha na kuwanyanyasa na kusababisha kukosekana kwa usalama, ustawi na maendeleo ya motto atachukuliwa hatua kali za kisharia ili kuhakikisha anakuwa mfano kwa watu waote watakaokiuka taratibu hizo.
“ Mtu yeyote atakayesababisha hatari ya usalama ,ustawi na maendeleo ya motto kwa makusudi hatutosita kumchukulia kupambana nae kwa njia zote na kumchukulia hatua kinidham na za kisheria sisi tunataka watoto wajisikie furaha, amani wawapo njiani, nyumbani, au shileni” Amesema Dkt. Mtahabwa
Awali Kaimu Katibu Tawala mkoa wa kigoma Bi. Paulina Ndigeza ameshukuru na kumpongeza Dkt. Lyabwene Mtahabwa kuwa mgeni rasimi katika Hafla hiyo na kusema Mkoa wa kigoma inao watoto wanaosoma katika shule jumuishi huku akiahidi mkoa wa kigoma na mikoa mingine mitatu iliyoteuliwa kufanya utafti huo kuwa wataufanyia kazi vizuri.
“Kwanza nikupongeze kwa kukubali mwaliko huu wa kuja kuwa mgeni rasmi katika hafla hii na umejionea mengi yaliyooneshwa na watoto mbele yako hapa mkoa wa kigoma ni miongoni mwa mikoa mine iliyoteuliwa kufanya utafti huu na kama ulivyoona tunao watoto wanaosoma katika shule jumuishi umeona ushuda wa mwanafunzi aliyekuja kutoa ushuda kutoka shule ya Sekondari Kigama Grand hivyo tukuahidi tu tutaenda kulifanyia kazi hili” Amesema Bi. Ndigeza.
Katika hatua nyingine Ndize Juma ambaye ni mwanafunzi mwenye ulemavu kutoka shule ya Sekondari Kigoma Grand amesema wananchi na jamii kwa ujumla wanapaswa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu hasa katika swala la elimu.
Mpango wa Programu ya Utafiti Tatuzi Kuhusu Usalama Jumuishi katika Elimu umezinduliwa leo chini ya taasisi ya Elimu Bora nchini ikiwa na lengo la kuwasaidiwa watoto wote nchini wenye ulemavu na wasio na ulemavu wanapata elimu bora bila changamoto yoyote ya unyanyapaa pamoja na ukatili juu yao.
Imeandikwa na Sharifat Shinji
0 Comments