Kasulu yatekeleza Ilani kwa kishindo

Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Isack Mwakisu amesema kuwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM umefanikiwa kwa aslimia kubwa katika kusimamia sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Miundombinu ya barabara, Kilimo, Ulinzi na usalama pamoja na Mfuko wa maendeleo ya jamii.

Amesema hayo machi 24, 2025 wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya CCM wilaya ya kasulu kwa mwaka 2020 hadi mwezi 2025 mwezi Februari mbele ya halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi wilaya ya Kasulu

Kanal Mwakisu ameongeza kuwa katika utekelezaji wa ilani ya chama hicho kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imefanikiwa kuimariha ulinzi kwa wananchi kwa kupambana na ramli chonganishi pamoja na uharifu wa kishirikina maarufu kamchape ambayo iliongeza migogoro baina ya wananchi katika wilaya hiyo.

“katika wilaya ya kasulu hali ya usalama ni ya kutosha licha ya kuwepo kwa matukio machache ya uhaifu hasa katika kipindi cha nyuma kidogo kuliibuka ramli chonganishi maarufu kamchape ambapo ilileta migogoro mingi baina ya wananchi na kutokuelewana lakini vilidhibitiwa na kuhakikisha usalama katika maeneo yote ya Kasulu” Ameongeza Kanal Mwakisu

Baadhi ya viongozi wa CCM wakishiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Kasulu

Kwa upande wa wajumbe wa mkutano huo wamesema kuwa katika miaka mitano ya utekelezaji wa ilani hiyo imefanikiwa kuboresha miungombinu mbalimbali ikiwemo barabara na huduma za maji.

“Ilani hii ilibeba maono yetu na utekelezaji wa miaka hiyo mitano tumeona kwa kiasi kikubwa mabadiliko makumbwa ya sekta miundombinu hasa kwa upande wa barabara na huduma muhimu ya maji mabadiliko makubwa yameonekana” wamesema baadhi ya wajumbe.

Wakati huohuo pia wajumbe hao wameongeza kwa kuomba serikali ya wilaya kuongeza juhudi za kukamilisha miradi kwa wakati ambayo bado haijakamilika kwa asilimila zote kulinagana na ukosefu wa pesa kutokufika kwa wadhabuni.

“kuna baadhi ya miradi ambayo bado haijakamili katika kata mbalimbali hutokana na wadhabuni kutoingiziwa pesa kwa wakati mfano barabara ya kata ya Kitagata na Kumnyika barabara zile hazipitiki katika kipindi hiki cha masika kutokana na kutokukamilika kwake”wameongeza wajume wa Mkutano.

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya Kanali Mwakisu amehitimisha kwa kuwataka wananchi wa wilaya ya Kasulu kuwa na tahadhari kutokana na ugonjwa wa Homa ya nyani (M-pox) ambao umeripotiwa kuingia katika wilaya ya Kasulu.

“kulingana na mazingira tunayoishi inabidi tubadili mtindo wa maisha ili kujiepusha na ugonjwa huu wa Homa ya nyani (M-pox) kutoka nchi jirani ambao mpaka hivi sasa tayari umeripotiwa kuingia nchini na katika wilaya ya kasulu pia upo kwaiyo Tujihadhari sana”Amesema Kanali Mwakisu. 

Katika utekelezaji wa ilani ya chama hicho kuna baadhi ya changamoto zilijitokeza ambazo zilikwamisha kukamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na uwepo wa imani za kishirikiana hali iliyohatarisha usalama katika halmashauri hiyo, kupanda kwa bei ya vifaa vya viwandani vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinuuvamizi wa ardhi na uchomaji wa misitu na kuchelewa kwa mapokezi ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.


Post a Comment

0 Comments