Tarime yaokoa jamii kwa kujenga daraja

 


Wananchi wa mtaa wa Kinyambi kata ya Nkende wameishukuru serikali ya halmashauri ya mji Tarime kwa kutumia mapato ya ndani kujenga daraja ambalo ni kivuko kutoka kata ya Nkende kwenda kata ya Nyandoto kupitia mto Moli.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mwenyekiti wa mtaa wa Kinyambi Mhe. Alphonce Ishengoma amesema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo matukio mengi yalikuwa yakitokea hasa katika kipindi cha masika.

"kiukweli hali ilikuwa ni mbaya sana kiasi kwamba nyakati za masiki zikifika kama wakati huu ni lazima uhai wa mtu ungepotea na mifugo pia kwa sababu maji yalikuwa yanajaa sana watu wanashindwa kuvuka" Amesema mwenyekiti Ishengoma

Aidha mwenyekiti huyo amewataka wananchi kulitunza daraja hilo pia amewaasa waendelee kulipa kodi kwani daraja hilo limejengwa kwa kupitia kodi ambazo wananchi wanalipa na pia kufanya kazi kwani kwa sasa daraja lipo .

"kwa sasa wananchi wanaweza kuvuka kwenda upande mwengine bila shida yoyote ni wakati mzuri kwaajili ya kutumia daraja hii kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali kuna baadhi ya watu walikuwa wanashindwa kusafirisha bidhaa sasa bidhaa zinafika" Amesema Ishengoma

Daraja la Mto Moli wilayani Tarime  mkoani Mara ambalo limejengwa kwa fedha kutoka katika mapato ya  ndani

Pia nao baadhi ya wananchi wa mtaa huo wameishukuru serikali kwa kujenga daraja hilo, hali ambayo imepelekea shughuli zingine za kiuchumi na kijamii kuendelea kwani kwa sasa wanatumia gari au pikipiki kusafiria bila kujali kiangazi au masika.


Post a Comment

0 Comments