Wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kigoma wamekutana na wenzao kutoka chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD katika mji wa Nyanzalaki Mkoa wa Makamba ili kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu.
Katibu wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT katika mkoa wa Kigoma Sarah Kairanya amesema wameamua kukutana na wanawake wenzao kwa kuwa wanaamini zipo changamoto za pamoja ambazo zinaweza kusaidia kuboresha maisha ya mwanamke.
Amesema kongamano hilo la kimataifa linazungimzia masuala ya uongozi na mwanamke, fursa na kiuchumi kwa wanawake ili kuwawezesha wanwake kutumia fursa kujiendeleza nje ya mipaka yao.
Kongamano hili ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani ambayo yanafanyika Machi 8 mwaka huu.
Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake wamekuwa na desturi ya kukutana na vyama rafiki katika nchi za Afrika mashariki na kusini mwa Afrika kwa ajili ya ujirani mwema na ukuzaji wa demokrasia
0 Comments