Wananchi wajitolea kujenga kituo cha Afya Kasulu DC

Katika hali ambayo ilianza kusahaulika nchini Tanzania, wananchi wa kijiji cha Kagerankanda wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamejitokeza kufanyakazi ya kusafisha bila malipo eneo kitakapojengwa kituo cha afya cha Kata ya Kagerankanda. 

Zoezi hilo limefanyika jana katika Kata hiyo ambayo haina kituo cha afya licha ya kjwa mbali kwa taribani KM 50 kutoka kilipo kituo cha afya Nyakitonto

Wakiongea na mwandishi wananchi wamefurahishwa na kitendo cha Serikali kuwatengea eneo kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya wakikiri kuwa kituo kikijengwa kitapunguza adha na athari za kupata huduma za afya.

“ Kwa kweli tumefurahia Serikali kututengea eneo kwa ajili ya kituo cha Afya kwani tulikuwa tunapata changamoto hasa tunapoandikiwa kwenda kujifungulia kituo cha Afya cha Nyakitondo walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kwa ajili ya huduma ya kujifungiua” Amesema Sung’ho Magembe.

“Nilisikia tangazo la kuja kujitolea kufanya usafi katika eneo hili hivyo wananchi wenzangu nawaomba tu waendelee kujitolea pia tunaiomba serikali itusapoti ili tuendelee kufanya kazi huku tukijuwa serikali inatushika mkono katika swala hili la ujenzi wa zahanati” Amesema Ivo Samason.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kusafisha kiwanja cha ujenzi wa kituo cha afya Kagerankanda, Kasulu


Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Kagerankanda Hereman Mtibilo amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika shughuli hiyo ya kijamii ya kufanya usfi katika eneo la ujenzi wa kituo cha Afya kata ya Kagerankanda na kuiomba serikali kuwatumia wataalamu kwa ajili ya kupima eneo pamoja na Gari kwa ajili ya kubebea mawe ambayo tayali wameshakusanya.

“Tukio hili limekuwa kubwa wananchi nawashukuru sana na siku ya Juma Tano ni siku ya kuja kuchimba Mawe kwa ajili ya msingi hivyo kituo hiki kikikamilika kitasaidia kwa kiasi kikubwa kwani kwa sasa wakinamama wanapangiwa kwenda kujifungulia Nyakitondo jambo ambalo sio zuri, serikali tunaiomba itushike mkono kwa kwa kutuletea wataalam kwa ajili ya Vipimo na Gari kwa ajili ya kubebea mawe” Amesema Mwenyekiti Mtibilo.

Aidha Mtendaji wa kijiji cha Kagera Nkanda Bw. Sabasi Boniphas amesema wananchi wamejitokeza kwa wingi katika zoezi hilo na kuwaomba wananchi waendelea kushiriki zoezi hili bila kushurutishwa na uongozi wa Kata.

“ Mwamko umekuwa mkubwa sana na nimewambia waandike majina yao waliojitokeza na baada ya hapa nitafanya msako kwa wale waliokaidi kuja katika zoezi hili, serikali kupitia mkurugenzi na mkuu wa Wilaya watushike mkono katika jambo hili ili tuweze kukamilisha zoezi hili, ni Muda mrefu tulipaswa kuwa na kituo cha Afya katika kata hii ya Kagerankanda” Amesema Mtendaji Bw. Sabas.

Ujenzi wa kituo cha Afya katika kata ya Kagera Nkanda linatekelezwa na Halmahauri ya wilaya ya Kasulu ambapo wananchi watachangia nguvu kazi na za a za ujenzi hususani Matofari , mchaga na Mawe.

Imeandikwa na Mwandishi wetu, Kagera Nkanda, Kasulu DC.


Post a Comment

0 Comments