*Waziri Dk.Ndumbaro akitangaza kiama kwa Maprofesa, Madaktari wanatakao husishwa migogoro ya ardhi Kagera*
Na. Mwandishi wetu, Bukoba
Waziri wa katiba na sheria Dk.Damas Ndumbaro ametangaza kiama kwa baadhi ya wasomo,maprofesa na madaktari wanaosababisha migogoro kwenye jamii hasa ile ya ardhi kuwakandamiza wananchi wa kipato cha chini kwenye jamii katika kesi zinazokuwa zikiwakabili.
Akizungumza na mwananchi Digital leo jumatatu,14,2025 akiwa mkoani Kagera Dk.Ndumbaro amesema wizara kupitia kampeni mbali mbali wamepita mikoa 24 wakisuruhisha na kutatua migogoro kwenye jamii huku wakijifunza zaidi ili watakapofika katika mkoa huo wajue jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo mara nyingi zinazosababishwa na maprofesa pamoja na madaktari.
"Kupitia kampeni zetu tulizofanya kwenye mikoa ya kutatua migogoro na kesi kwenye jamii, ikiwemo ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia tulikuwa tukijifunza endapo tukifika mkoa Kagera mkoa wenye wasomi wengi na maprofesa tutakabiliana vipi"
Amesema wizara ya katiba na sheria wamejipanga kutokemeza migogoro ya ardhi,Mirathi,na ndoa ukatili wa kijinsia na ipo taarifa za migogoro na kesi nyingi na kusababishwa na baadhi ya wasomi kama maprofesa na madaktari kuwakandamiza wananchi wa kipato cha chini.
"Kwa mfano kule Kanyigo kuna maprofesa wengi kama kuna migogoro sasa tuko tayari kwenda huko kuhakikisha wananchi wanapata Haki"amesema Dk.Ndumbaro
Mkuu wa mkoa Kagera, Fatma Mwassa akiongelea walivyojipanga kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wanajihusisha kwenye migogoro
Takwimu kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera zinaonyesha uwepo mkubwa wa changamoto ya migogoro na kesi zinazohusu ardhikwa wingi ambapo migogoro 200 kila wiki kuripotiwa kwenye mabaraza ya ardhi.
Mara nyingi zinaonyesha watu wenye kipato cha juu,wasomi maprofesa na madaktari wakiwafikisha kwenye mabaraza na mahakama wananchi wa kipato cha chini.
Aidha,Dk.Ndumbaro amewatahadharisha wanasiasa wenye tabia ya kutaka kuwq viongozi na kusababisha maandamano yasiyo na utaratibu wa kisheria na kikatiba kuwa wizara haitasita kuwachukuli hatua.
Amegusia wanasiasa hivi karibuni ambao hawana niya nzuri kwa wananchi waliyohusishwa kuandaa maandamano na kushawishi wananchi kutoshiriki uchaguzi mkuu mwaka huu mwezi octoba,2025 huku akitaja mihimili ya kutatua changamoto na kutangaza kuwa hili jambo lisifanyike kikatiba kuwa ni Serikali,Bunge na chama kilichopo madarakani.
"Wewe unaandaa maandamano na kuleta migomo kwa wananchi wewe ni nani"mimi kama waziri wa katiba na sheria nijukumu langu kusimamia sheria na vifungu vyake hatuko tayari kuhatarisha matatizo kwenye nchi"
Kwa upande wa mkuu wa Kagera,Fatma Mwassa amesema taarifa za migogoro mara nyingi imewahusisha hadi viongozi wa serikali za mitaa katika mkoa huo kama vile wenye viti na watendaji.
Amesema kama mkoa wamejipanga vizuri kupitia wataalamu wa kisheria mwenyekiti au mtendaji na watumishi yeyote atakayebainika kwenye kesi au mgogoro hawatasita kuwavua vyeo na kuwachukulia hatua.
Pamoja na makalipio hayo, Mkoa Kagera leo, umezinduwa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia lengo ikiwa nikutaka kuwasaidia wananchi kupata usawa na haki kwenye migogoro nakesi zinazowakabili bure.
0 Comments